Kiswahili
Msaada - Rejesha katika Firefox
Urejeshaji wa vichupo vya Firefox vilivyopotea

Ikiwa umepoteza vichupo vyovyote vya OneTab ndani ya Firefox, tunaomba radhi sana kuhusu hili. Mara chache, wasifu wa Firefox unaweza kuharibika.

Hata hivyo bado kuna tumaini. Kuna uwezekano mkubwa kuwa vichupo vyako vinaweza kurejeshwa kwa urahisi, aidha kwa Windows System Restore, Mac Time Machine, au kupitia Mtoa Hifadhi Rudufu Mtandaoni iwapo unatumia mmoja.

Kabla hujaanza: Tafuta folda ya wasifu wa Firefox kisha itengenezee nakala

Firefox huhifadhi mipangilio yako yote (pamoja na data ya OneTab) katika "folda ya wasifu". Ili kupata folda hii, kwanza fungua Firefox. Kutoka kwenye menyu ya "Msaada", chagua "Troubleshooting Information". Kichupo cha "Troubleshooting Information" kitafunguka. Chini ya sehemu ya "Application Basics" karibu na "Profile Folder", bofya "Show in Finder" (Mac) / "Open Folder" (Windows). Dirisha litaonekana lenye folda yako ya wasifu.

Kabla ya kuendelea, funga Firefox na utengeneze nakala ya folda hii ya wasifu. Hii itamaanisha unaweza kurejesha folda ya wasifu ya Firefox iwapo kitu kitaenda vibaya. Kumbuka kuwa unapotekeleza maagizo yafuatayo ya kurejesha hifadhi rudufu, data mpya zaidi ya Firefox (kama alamisho au historia ya kuvinjari ya karibuni) itaondolewa kwa kuwa unarejesha data ya zamani ya Firefox.

Maagizo ya Windows Backup / Windows System Recovery

Windows huenda ilitengeneza hifadhi rudufu ya kiotomatiki ya folda ya wasifu wa Firefox.

1. Bofya-kulia folda ya wasifu wa Firefox na uchague "Properties". Bofya kichupo cha "Previous Versions" kisha subiri Windows ionyeshe matoleo ya awali ya folda hiyo. Ikiwa hakuna "Previous Versions", basi ikiwa una aina yoyote ya mfumo wa hifadhi rudufu (kama usajili wa hifadhi rudufu mtandaoni) kwenye kompyuta yako tafadhali ruka hadi sehemu inayofuata (maagizo ya Windows Online Backup).

2. Chagua toleo la awali kutoka tarehe ya mwisho kabla hujapoteza vichupo vyako. Bofya kitufe cha "Restore" na uandike juu ya folda yako ya sasa ya wasifu wa Firefox.

Maagizo ya Windows Online Backup

Ukitegemea aina yoyote ya mfumo wa hifadhi rudufu, kama mfumo unaohifadhi mara kwa mara yaliyomo ya kompyuta yako mtandaoni, tafadhali jaribu hatua hizi:

1. Ingia kwa mtoa huduma wako wa hifadhi rudufu mtandaoni au mfumo mwingine wa hifadhi rudufu, na uone kama umehifadhi folda ifuatayo:
C:\Users\Username\AppData\Roaming\Mozilla\Firefox\Profiles\Profile Folder
(ambapo "Profile Folder" itakuwa folda yenye msururu wa nasibu wa herufi kama jina, k.m. "abcdef12.default")

2. Rejesha folda hii, ukiandikiza juu ya folda yako ya sasa ya wasifu wa Firefox.

Maagizo ya Mac Time Machine

Vichupo vinaweza kurejeshwa kwa kutumia mfumo wa ndani wa Time Machine:

1. Fungua programu ya Time Machine (iliyo kwenye folda ya Applications), nenda kwenye diski kuu yako (kawaida huitwa Macintosh HD), kisha nenda kwenye hifadhi rudufu ya folda ya wasifu iliyo kwenye: /Users/Username/Library/Application Support/Firefox/Profiles/Profile Folder
(ambapo "Profile Folder" itakuwa folda yenye msururu wa nasibu wa herufi kama jina, k.m. "abcdef12.default")

3. Ukilitumia kitelezi ndani ya Time Machine, rudi nyuma hadi tarehe kabla hujapoteza vichupo vyako.

4. Ukifika hapo, bofya-kulia folda ya wasifu na uchague "Restore Profile Folder to..." kisha uandikize juu ya folda yako ya sasa ya wasifu wa Firefox.

Maagizo ya Mac Online Backup

Ukitegemea aina yoyote ya mfumo wa hifadhi rudufu, kama mfumo unaohifadhi mara kwa mara yaliyomo ya kompyuta yako mtandaoni, tafadhali jaribu hatua hizi:

2. Ingia kwa mtoa huduma wako wa hifadhi rudufu mtandaoni au mfumo mwingine wa hifadhi rudufu, na uone kama umehifadhi folda ifuatayo:
/Users/Username/Library/Application Support/Firefox/Profiles/Profile Folder
(ambapo "Profile Folder" itakuwa folda yenye msururu wa nasibu wa herufi kama jina, k.m. "abcdef12.default")

3. Ndani ya mfumo wa hifadhi rudufu mtandaoni, tafuta toleo la folda hii lililohifadhiwa kabla ya tarehe uliyo poteza vichupo vyako. Rejesha folda hii na uandikize juu ya folda yako ya sasa ya wasifu wa Firefox.